Wednesday, May 30, 2012

Zitto: Tawi letu sio la kupanga `dili`


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema tawi la chama hicho lililozinduliwa Washington nchini Marekani sio kijiwe cha kupanga madili bali kisima cha fikra na mawazo ya kujenga nchi.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, aliyasema hayo jijini Washington alipokuwa akizindua tawi la Chadema nchini humo.

Alisema lengo la matawi hayo ni kupata fikra na mawazo yatakayoisaidia nchi na sio sehemu ya kufanya majungu ya kudanganya viongozi wakuu wa nchi wanaokwenda nchini humo.

“Matawi ya Chadema Washington DC sio kama ya CCM ambayo yakikaa yanawaza rais au waziri mkuu akija wamdanganye nini, wapeleke umbea gani au ‘kuchomana’ Watanzania wenyewe kwa wenyewe…hatutaki hayo; tunataka yawe kisima cha fikra na mawazo ya kuiendeleza nchi,” alisema.
Katika uzinduzi huo, Watanzania kadhaa waishio Marekani walichukua kadi za Chadema.

Naibu katibu mkuu wa chadema Zitto Kabwe akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Kalley Pandukizi.

0 comments:

Post a Comment